Na Dkt. Canberth Tibihika.
SHINIKIZO la damu kwa muda mrefu limekuwa likionekana kama ugonjwa unaowapata watu wazee. Hata hivyo, hali hii inabadilika kwa kasi. Kila siku, watuwalio chini ya umri wa miaka 40 wanagundulika kuwana shinikizo la damu, mara nyingi bila wao kujua hadi matatizo makubwa yatokee.
Mabadiliko hayo kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mtindo wa maisha wa kisasa, ikiwa ni pamoja na ulaji usio bora, muda mrefu kazini, msongo wa mawazo, kutofanya mazoezi yamwili, na ulaji mkubwa wa vyakula vilivyosindikwa viwandani.
Kinachofanya shinikizo la damu kuwa hatari zaidi ni jinsi linavyoendelea kimya kimya. Mara nyingi huitwa “muuaji wa kimya” kwa sababu halina dalili za wazi katika hatua zake za mwanzo. Vijana wengi hujisikia wako salama, hata kama viwango vyao vya shinikizo la damu viko juu sana.
Akifafanua zaidi Meneja Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja kutoka Jubilee Health Insurance anaeleza kwamba bahati mbaya, hiyo inamaanisha kuwa tatizo hili hugundulika tu baada ya kusababisha madhara makubwa kwenye moyo, figo, au viungo vingine muhimu.
Anasema kugundua mapema ni moja ya njia bora zaidi za kudhibiti na kuzuia madhara ya muda mrefu ya shinikizo la damu. Vipimo vya mara kwa mara vya afya, ikiwemo kupima shinikizo la damu, vinapaswa kuwa sehemu ya kawaida ya utunzaji wa afya kwa watu walio kwenye umri wa miaka ishirini na thelathini.
“Dalili ndogo kama maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, uchovu usioelezeka, maumivu ya kifua, au mabadiliko katika kuona yanaweza kuwa ishara za mapema zinazohitaji uangalizi wa daktari.
“Jubilee Health Insurance imejizatiti kusaidia watu kutambua na kudhibiti hali za kiafya kabla hazijawa kubwa.
“Mipango yetu ya afya inagharamia vipimo muhimu, ushauri wa madaktari, na dawa kwa wale wanaoishi na shinikizo la damu. Tunatambua kuwa uthabiti ni muhimu katika kudhibiti magonjwa ya muda mrefu.
“Ndiyo maana tunatoa huduma ya Jubilee Health Drug Delivery, inayo hakikisha dawa zilizo orodheshwana daktari zinapelekwa moja kwa moja kwa wateja wetu. Huduma hii husaidia kufuata matibabu kwa ufasaha na pia kupunguza usumbufu wa kwenda mara kwa mara dukani, hasa kwa watu wenye ratiba ngumu.”
Ameongeza kuwa habari njema ni kwamba shinikizo la damu mara nyingi linaweza kuzuiwa au kudhibitiwa kwa msaada wa kitabibu na mabadiliko ya mtindo wa maisha. Kufanya maboresho madogo lakini ya kila mara katika maisha ya kila siku kunaweza kuleta matokeo makubwa kwa muda mrefu.
Amesema kula chakula bora chenye mboga nyingi za majani, matunda, nafaka zisizokobolewa, na protini zisizo na mafuta husaidia kupunguza shinikizo la damu kwa asili. Kupunguza ulaji wa chumvi, sukari, na vyakula vilivyosindikwa pia ni muhimu.
Pia mazoezi ya mwili pia yana mchango mkubwa. Kufanya angalau dakika 30 za mazoezi ya wastani kila siku, iwe ni kutembea, kuendesha baiskeli, kuogelea, au kucheza muziki, huboresha sana afya ya moyo na mishipa ya damu.
Aidha, kupata njia bora za kupunguza msongo wa mawazo kama mazoezi ya utulivu wa akili, kuandika shajara, au kupata ushauri nasaha kunaweza kusaidia zaidi katika kudhibiti shinikizo la damu.
Matumizi ya pombe na tumbaku yanapaswa kupunguzwa, kwani yote yanajulikana kuongeza shinikizo la damu na hatari ya matatizo yanayohusiana. Usingizi, ambao mara nyingi hupuuzwa, ni kipengele kingine muhimu cha afya ya moyo. Kipaumbele cha kupata saa saba hadi nane za usingizi mzuri kila usiku huchangia kwa ustawi wa jumla.
Shinikizo la damu si lazima liwe kizuizi katika maisha yako. Ukiwa na uelewa, uchunguzi wa mapema, na mfumo sahihi wa msaada, vijana wanaweza kudhibiti afya yao. Jubilee Health ipo pamoja nawe katika safari hii, tukihakikisha unaishi sio tu maisha marefu bali pia yenye nguvu, ukiwa na moyo ulio tayari kwa kila kitu kinachokuja maishani.