Mjumbe wa INEC ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya leo jijini Arusha.
Mjumbe wa INEC ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya leo jijini Arusha .
…………….
Happy Lazaro, Arusha
WARATIBU wa uchaguzi , wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo wamekutana jijini Arusha kwa siku tatu kwa ajili ya mafunzo ikiwa ni maandalizi ya kuwawezesha kutekeleza ipasavyo kazi na jukumu lililo mbele yao.
Akifungua mafunzo hayo leo Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi ,Dkt.Zakia Abubakar amesema kuwa ,wameteuliwa kwa mujibu wa Sheria na tangu tarehe ya uteuzi wao wana wajibu wa kikatiba na kisheria kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais ,wabunge ,madiwani kwa Tanzania bara kwa niaba ya Tume katika maeneo yao ya uteuzi.
Amesema kuwa, dhamana waliyopewa ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi ni nyeti na muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu hivyo wanategemewa kwa kuzitambua utendaji wao.
Aidha amewataka kuwajibika ipasavyo katika kipindi chose cha utumishi wao wa Tume hadi hapo watakapokamilisha jukumu hilo la uchaguzi mkuu.
Amesema kuwa ,mafunzo hayo yanajumuisha washiriki 86 kutoka mikoa ya Arusha ,Manyara ambao ni waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ,maafisa uchaguzi na maafisa ununuzi.
“Mafunzo haya yanafanyika kwa wakati mmoja katika mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya,Mwanza,Shinyanga,Ruka na Kusini Pemba .”amesema .
Ameongeza kuwa, mada kumi na mbili zitawasilishwa ambapo pamoja na mambo mengine watapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kujadiliana namna ya kufanikisha uchaguzi katika maeneo yao na kujadili namna ya kukabiliana .na changangamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi.
” Natumia nafasi hii kuwaasa pamoja na uzoefu ambao baadji yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi msiache kusoma katiba,Sheria, kanuni,taratibu,miongozo na fuateni na tekelezeni maelekezo mbalimbali yatakayokuwa yanatolewa na Tume .”amesema.
Aidha Dkt .Zakia amewataka kusoma kwa umakini katiba, Sheria, kanuni miongozo na maelekezo mbalibali yaliyotolewa na yatakayotolewa na Tume na ulizeni ili mpate kufafanuliwa kwenye maeneo ambayo kwa namna moja au nyingine yatakuwa na changamoto za kufahamu ili kuwarahisishia katika utekelezaji wao wa kazi za uchaguzi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Tume ya uchaguzi, Jafari Makupula amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa na uwezo wa kusimamia shughuli za uchaguzi .
Amesema kauli mbiu ya uchaguzi mkuu mwaka huu ni “kura yako ,haki yako jitokeze kupiga kura “