Jaji wa Mahakama Kuu na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Asina Omari akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza.
………………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Waratibu wa uchaguzi wa mikoa,wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Jimbo,maafisa uchaguzi na maafisa ununuzi wameaswa kuhakikisha wanasimamia rasilimali vifaa watakavyopewa katika utekelezaji wa kazi za uchaguzi hatua itakayosadia zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.
Hayo yamebainshwa leo Julai 23, 2025 na Jaji wa Mahakama Kuu na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya UchaguI (INEC), Asina Omari wakati akifunga mafunzo ya Sheria,Kanuni,maelekezo mchakato na taratibu za uchaguzi kwa wasimazi hao yaliyofanyika kwa siku tatu Jijini Mwanza.
Ameeleza kuwa ili zoezi la Uchaguzi Mkuu lifanyike vizuri ni lazima wasimazi wahakiki vifaa vya uchaguzi mara tu watakapopewa na kuhakikisha wanatoa taarifa haraka iwapo kunaupungufu wowote.
Aidha, amewaasa kusimamia vyema matumizi ya fedha watakazotumiwa kwaajili ya shughuli za uchaguzi.
Mwisho aliwakumbusha kusimamia mafunzo waliyofundishwa na kuyaishi kwakuzingatia katiba,Sheria,Kanuni na maelekezo ya tume.
“Pelekeni elimu hii mliyoipata kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata na watendaji wa vituo vya kupigia kura kwa weledi ili uchaguzi uweze kufanyika vizuri”, amesema Jaji Omari.