Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikaribishwa kwa utamaduni wa watu wa Belarus alipoingia kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya President iliyopo jijini Minsk nchini Belarus, kuzungumza na wawakilishi wa Muungano wa kampuni za Belarus zinazofanya Biashara na mataifa ya Afrika (AFTRADE), Julai 23, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi na Belarus, Frederick Kibuta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na wawakilishi wa Muungano wa kampuni za Belarus zinazofanya Biashara na mataifa ya Afrika (AFTRADE) baada ya kuzungumza nao kwenye hoteli ya President ya jijini Minsk nchini Belarus, Julai 23, 2025. Wa tatu kulia ni Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Sariff Ali Shariff, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Khatibu Kazungu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiendesha trekta la mafunzo alipotembelea Chuo Kikuu cha Kilimo Belarus (BSATU) jijini Minsk Julai 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama trekta kubwa na la kisasa alipotembelea Chuo Kikuu cha Kilimo Belarus (BSATU) jijini Minsk, Julai 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Belarus (BSATU) jijini Minsk alipokitembelea, Julai 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Kilimo Belarus (BSATU) jijini Minsk baada ya kukitembela, Julai 23, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)