Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link Ltd, Abdul malik Mollel akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kuhusu maonesho hayo.
……..
Happy Lazaro, Arusha.
Taasisi ya uwakala wa vyuo vikuu vya nje Global Education Link Ltd imeandaa maonesho ya elimu ya vyuo vikuu nje ya nchi yanayofanyika katika Hotel ya Fourpoints hotel iliyopo jijini Arusha .
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Global Education Link Ltd, Abdul malik Mollel akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha kwenye maonesho hayo amesema kuwa taasisi hiyo inajihusisha na elimu ya juu nje ya nchi ambapo huu ni mwaka wa 18 sasa .
“Leo tupo katika maonesho haya ya elimu ya kimataifa hapa Arusha katika Hotel ya Fourpoints hotel kwa lengo la kukutana na wanafunzi pamoja na vijana wenye uhitaji wa kutaka kusoma nje lakini walikuwa hawajui pa kuanzia
“amesema Mollel.
Amesema kuwa kazi yao kubwa ni kuwapa fursa vijana wa kitanzania kwenye upande ushauri katika ndoto zao and guidance.
“Kijana yoyote ama mzazi anayekuja katika maonesho haya kwanza atapata ufahamu juu ya kozi gani anataka kusoma je unafikia vigezo kuhusu historia ya elimu aliyo nayo na kumsaidia kuchagua kozi katika nchi ambayo angeipenda ,chuo ambacho tungependa kumpa na angekihitaji kwa gharama ambayo ni nafuu .”amesema .
Ameongeza kuwa ,wale vijana au mabinti ambao wamemaliza kidato cha nne au sita ama amemaliza diploma amepata matokeo yake au anategemea kumaliza aidha diploma au degree na ana uhitaji wa kupata chuo bora nje ya nchi.
“Tunatoa udahili wa hapo kwa hapo mwanafunzi anayekuja humu ndani udahili wa chuo kikuu ndani ya dakika 15 zinaanza kutoka na ndani ya masaa 24 wanafunzi wa Arusha wanapata udahili.”amesema Mollel .
Amesema kuwa ,udahili huo ni wa kozi za uinjinia ,kozi za afya ,kozi za arts na kozi zote za biashara katika level zote za cheti,diploma, digrii, masters na PhD.
Hili ni jambo kubwa sana ambalo wananchi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara ,Singida wanapata huduma hizo.
“Jambo la.muhimu kwa hapa Arusha ni fursa sio tu kusoma lazima ujue unasoma katika chuo kipi na chenye fursa zipi ili mbele ya safari unapomaliza chuo mode ya ufundishaji wao uonekane pia kuwa swala la fursa za kazi ama kujitegemea .”amesema .
“Kwa mfano mwanafunzi yoyote anayetaka kusoma master ama PhD ada ya shule sifuri yaani yeye halipi ada ni safuri ila atalipa.hostel pamoja na gharama zake za chakula ambazo ni dola 1500 sawa na shs 4 milioni kwa mwaka lakini ada ya shule ni ziro kwa master hiyo ni fursa .”amesema .
Ameongeza kuwa,kama mwanafunzi anataka kusoma kozi ya udaktari ,injinia tunachokifanya ni gharama zipo lakini ni asilimia 50 ufadhili kozi zote katika maonyesho haya kwa hiyo mtu.yoyote anayefika hapa kama wanahitaji kupata fursa za kuendeleza taaluma zao nje ya nchi vyuo vikuu hivi ambavyo vipo hapa vina specilization kwenye taaluma mbalimbali ikiwemo ya wanahabari pia huku wakiangalia na uzoefu uliona nao haya mambo matatu tumeyaleta katika mkoa wa.Arusha .
“Tunashukuru idadi ya wanafunzi imekuwa kubwa sana mwitikio umekuwa mkubwa sana “amesema Mollel .
Nao baadhi ya Wazazi na wanafunzi waliofika katika maonyesho hayo,Daniel Kaaya amesema kuwa,kitendo hicho kilichofanywa na Taasisi hiyo ni muhimu sana kwani wanapata fursa ya kuhudhuria na kufahamu maswala mbalimbali ya vyuo vikuu nje ya nje ambavyo walikuwa hawavijui kabisa .
“Kwa kweli imekuwa fursa kubwa sana kufahamu na kuweza kujiunga na vyuo vya nje ya nchi kwani wameleta hadi wamiliki wa vyuo hivyo kutoka nje ya nchi kitendo ambacho ni kizuri sana na fursa hii inatakiwa kuchangamkiwa sana hasa kwa vijana wa kitanzania .”amesema .
Mmoja wa wanafunzi wa chuo ,Nancy Augustino amesema kuwa, amefurahi sana kwa kitendo cha Taasisi hiyo kuleta maonesho hayo kwani alikuwa na shauku kubwa ya kusoma nje ya nchi ila changamoto alikuwa hajui namna ya kupata mawasiliano hivyo anashukuru sana .
“Kwa kweli nashukuru sana kwani nimeweza kusaidika na kupata ufadhili wa kwenda kusoma India na ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu sana kufanya hivyo .”amesema.