LASSINE Kouma kapewa jezi namba 8 ambayo iliwahi kuvaliwa na mastaa wakubwa katika kikosi hicho akiwemo Haruna Niyonzima kiungo aliyekuwa anafanya watu wadhani mpira ni kazi rahisi.
Kouma mwenye miaka 21 anazima dili la Yanga SC kuiwinda saini ya Feisal Salum wa Azam FC ambaye ana nguvu kubwa katika mguu wake wa kulia.
Katika Ligi ya Mali alifunga jumla ya mabao 7 na kutoa pasi 6 za mabao alikuwa anakipiga ndani ya Stade Malien ni raia wa Mali.
Lassine ni namba 8 mpya wa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye ni kocha mpya mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi.
Baada ya utambulisho wake Yanga SC wamebainisha kuwa ambacho anahitaji ni kuona wanaendeleza moto wa kutembeza dozi ya 5G kwenye mechi za ushindani ndani ya uwanja.