Feisal Amekubali Kusaini mkataba wa awali wa miaka miwili na Simba SC lakini amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Azam FC.
Makubaliano ni kati ya Feisal na Simba mengine ni makubaliano ya klabu kwa klabu. Endapo Azam itakataa, Feisal atalazimika kujiunga na Simba SC mwakani mkataba wake utakapomalizika.
Kilichobaki ni Simba kufanya mazungumzo na Azam lli kuvunja Mkataba wa Feisal, lakini kumbuka, Azam wanaweza kukataa kumuuza mchezaji huyo, tusubiri tuone mwisho.