Mchezo ni mmoja tu akichukua wako na yeye chukua wakwake “piga panapo uma”
Mara baada ya Yangasc kufanya umafia kwa watani wao wa Jadi Simbasc kwa kumchoma Mohamed Hussen ambaye alikuwa tayari amemaliza mkataba wake na miamba hiyo ya soka
Mnyama nae bila ya kuchelewa ameamua kujibu kwa kishindo
Simbasc wameamua kuwekeza nguvu kwa mlinzi wa kati wa Yangasc Dickson Nickson Job ambaye na yeye amemaliza mkataba wake na mpaka sasa ajasaini mkataba mpya
Taarifa za ndani zinaeleza ya kwamba mwamba tayari ameweka dau lake mezani ambalo analitaka huku Yangasc wameonyesha kutokukubaliana na hilo dili na kuhitaji Dickson Nickson Job kushusha dau hilo
Huku mnyama ndiyo anatajwa kumpa kiburi hicho na tayari wameweka dau nono kuliko la Yangasc
Hii inatafsiriwa kama kisasi ambacho kitauma kwa Yangasc baada ya wao kufanikisha dili la Zimbwe Jr