Uongozi wa Singida Black umewafahamisha mashabiki, wapenzi na wadau wake juu ya kuridhia mshambuliaji Jonathan Sowah kusajiliwa Simba kwa makubaliano maalum.
Taarifa ya Singida Black Stars imeeleza kuwa, makubaliano hayo yamefikiwa baina ya mlezi wa klabu hiyo ya mkoani Singida na Rais wa heshima wa Simba pamoja na Uongozi wa klabu hizo.
Singida Black Stars imemtakia kila la kheri Jonathan Sowah katika changamoto mpya, na imemshukuru kwa kuitumikia vyema klabu hiyo katika kipindi chote.