Aliyekuwa kiungo mahiri wa Yanga SC, Khalid Aucho, ametoa kauli ya kushangaza kupitia TikTok Live baada ya kuachana rasmi na mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania Bara. Katika mazungumzo yake na mashabiki, Aucho alieleza kuwa hana tatizo lolote kujiunga na watani wa jadi wa Yanga, Simba SC, endapo watamwonyesha nia ya kumsajili.
“Hakuna shida kabisa, kama Simba watanihitaji basi nipo tayari kujiunga nao mara moja,” alisema Aucho akiwa mubashara mtandaoni.
:Kauli hii iliibuq mjadala mkali kwenye comments, hasa kwa mashabiki wa Yanga ambao walionyeshwa kutopendezwa na kauli hiyo. Aucho amekuwa sehemu ya mafanikio ya Yanga katika misimu ya hivi karibuni, akichangia kwenye ubingwa wa Ligi Kuu.
Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka Simba SC juu ya nia yao ya kumsajili kiungo huyo, lakini kwa kauli yake, Aucho ameweka wazi kuwa mlango uko wazi kwa upande wake.