Klabu ya Yanga imetangaza kumuongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wao raia wa DR Congo Maxi Mpia Nzengeli wa kuendelea kusalia kwa Mabingwa hao wa Nchi hadi mwaka 2027.
Nyota huyo alijiunga na wananchi mwaka 2023 akitokea Union Maniema inayoshiriki ligi kuu ya nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.