NIGERIA: Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Nigeria( Super Falcons), Asisat Oshoala, amekanusha tetesi zinazodai kuwa amejiondoa katika soka la kimataifa.
Mchezaji huyo bora wa Afrika mara sita alitoa ufafanuzi huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nchini Morocco kufuatia ushindi wa Nigeria wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2024.
Akijibu madai ya kustaafu, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alisema, “Sijui hiyo ilitoka wapi lakini ajenda lazima iandaliwe. Ninaipata, lakini sisumbuki. Bado niko hapa. Bado nacheza. Bado nafanya kazi yangu. Hilo ndilo ninalozingatia.”
Licha ya kutoanza mara kwa mara katika mashindano hayo, Oshoala alishiriki katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 cha Nigeria na alicheza na kuisaidia timu yake kufikia mafanikio ya kubeba kombe hilo.
Tangu alipocheza mechi yake ya kimataifa mwaka wa 2013, mshambuliaji huyo wa Barcelona ameandika jina lake katika vitabu vya historia, hasa baada ya kuibuka kidedea katika Kombe la Dunia la Wanawake U-20 2014 na Ubingwa wa Afrika kwa Wanawake wa mwaka huo huo.
Anasalia kuwa Mwafrika wa kwanza kufunga katika mashindano matatu mfululizo ya Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA na sasa anaongeza taji la nne la WAFCON kwenye mkusanyiko wake – akiwa ameshinda hapo awali 2014, 2016, na 2018
The post Oshoala azima uvumi wa kustaafu first appeared on SpotiLEO.