MUNICH: KWA mujibu wa mtaalamu wa taarifa za usajili wa wachezaji, Fabrizio Romano, Luis Diaz atasaini Bayern Munich ndani ya saa 24 zijazo, baada ya kukubali kuhama kwa pauni milioni 65 kutoka Liverpool.
Fabrizio Romano, amethibitisha kwamba Diaz ataondoka kwenye kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa Reds kukamilisha dili hilo.
“Mpango umethibitishwa kwa Luis Diaz: winga mpya wa Bayern atawasili leo mjini Munich na anatazamiwa kukamilisha vipimo kesho Jumanne Julai 29, 2025.
“Mkataba wa miaka minne utatiwa saini saa 24 zijazo,” Romano alichapisha kwenye ukurasa wake wa X.
Liverpool sasa wako tayari kuweka benki pesa za ziada kwa ajili ya harakati zao za kumpata Alexander Isak.
Winga huyo wa The Reds aliiambia Arne Slot mapema msimu huu wa joto kwamba alitaka kuondoka Anfield.
Diaz mwenye miaka 28, alijiunga na Liverpool alipokuwa barani Asia kwa ziara yake ya kujiandaa na msimu mpya lakini aliachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kirafiki dhidi ya AC Milan.
Na sasa Liverpool wamempa rasmi Diaz ruhusa ya kuondoka kwenye ziara hiyo baada ya kuafikiana na Bayern.
Mabingwa hao wa Premier League mara mbili walishindwa katika majaribio ya kumshawishi Diaz kusaini mkataba mpya.
Joao Felix kumfuata Ronaldo Al-Nassr
LONDON: MABINGWA wa kombe la Klabu Bingwa Duniani, Chelsea wamekubali mkataba wa pauni milioni 43.7 ili kumtoa mshambuliaji wao Joao Felix kwenda klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.
Felix, ambaye alijiunga na The Blues kutoka Atletico Madrid kwa uhamisho wa pauni milioni 38.4, alitatizika kufanya vyema wakati alipokuwa London.
Baada ya kipindi kibaya cha mkopo akiwa AC Milan katika kipindi cha pili cha msimu wa 2024-25, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno sasa yuko tayari kuungana na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr, kufuatia Benfica kushindwa kufikia thamani ya Chelsea.
Felix alishiriki katika mechi 12 pekee za Ligi Kuu msimu uliopita, akifunga mara moja pekee na alikuwa ametengwa kwa muda mrefu.
Kuondoka kwake kutatoa msukumo muhimu wa kifedha huku Chelsea wakiweka sawa vitabu vyao ili wasinase kwenye kanuni za kifedha za UEFA, tayari wametumia pauni milioni 169 kununua wachezaji wapya msimu huu wa majira ya joto.
Jackson anataka kucheza Manchester United
WAKATI zoezi la usajili wa wachezaji likiendelea kwa timu mbalimbali mchezaji Nicolas Jackson amevutiwa na Manchester United, wakati mchezaji Kiernan Dewsbury-Hall, aliyesajiliwa kutoka Leicester kwa pauni milioni 30, sasa analengwa kwa mkopo na Fulham, huku kukiwa na mkataba wa kudumu katika kazi hiyo.
Wakati huo huo, Renato Veiga anakaribia kuhamia Atletico Madrid. Timu hiyo ya Uhispania inajaribu kujadili bei ya Chelsea ya pauni milioni 35 hadi kufikia pauni milioni 25.
Kiungo huyo Mreno, ambaye alijiunga kutoka Basel kwa pauni milioni 11.7 na kucheza mara 18 msimu uliopita, ameonesha nia ya kutaka kuondoka klabuni hapo.
Raheem Sterling na Ben Chilwell pia wanachunguza chaguzi za kuondoka huku Chelsea ikijaribu kuboresha kikosi kilichojaa na kutii matakwa ya usajili ya UEFA ili kushiriki Ligi ya Mabingwa.
Newcastle, kwa upande wao, wanawania ofa muhimu. Ingawa wanasitasita kuuza, wanaweza kulazimika kufikiria kupokea pesa kutokana na masuala ya Financial Fair Play na ukubwa wa ofa inayotarajiwa ya Liverpool.
Liverpool kuvunja rekodi usajili wa Alexander Isak
TIMU ya Liverpool inaandaa dau la rekodi la klabu kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Newcastle United Alexander Isak huku wakiharakisha mipango ya kuchukua nafasi ya winga anayeondoka Luis Diaz, ambaye yuko mbioni kujiunga na Bayern Munich kwa pauni milioni 65.
The Reds wana nia ya kuwekeza tena fedha kutokana na kuondoka kwa Diaz, Isak ndiye ameibuka kama shabaha yao kuu ya ushambuliaji.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidish mwenye umri wa miaka 25 ameripotiwa kukataa nia ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, na kuweka wazi kwamba kipaumbele chake ni kusalia kwenye Ligi Kuu ya England haswa kucheza katika timu ya Livberpool ya Anfield.
Wadadisi wa mambo ya uhamisho wanaonesha kuwa Liverpool inakamilisha pendekezo la rekodi kwa Isak.
Hata hivyo, wataendelea pindi tu watakapopokea mwanga wa kijani kutoka kwa Newcastle, huku ripoti zikisema kuwa mshambuliaji huyo tayari ameiarifu klabu hiyo kuhusu nia yake ya kuondoka msimu huu wa joto.
Liverpool tayari wametumia takriban pauni milioni 300 dirisha hili chini ya meneja mpya Arne Slot, ikijumuisha mikataba ya Hugo Ekitike na Florian Wirtz.
Lakini pamoja na Diaz na Darwin Nunez wanaotarajiwa kuondoka, kuimarisha mstari wa mbele imekuwa muhimu.
The post TETESI ZA USAJILI MAJUU first appeared on SpotiLEO.