Zaka Zakazi🎙”Azam Haiwezi kumuuza Feisal kwenda Simba sababu Simba hiyo Pesa hawana, labda nikuambie mkataba wa Feisal unakipengele kama atauzwa kwenda Simba basi Yanga inabidi alipwe bilioni Moja (Yaani kwenye mkataba imetajwa kabisa Simba), sasa Simba atatoa shilingi ngapi ili Azam imlipe Yanga Bilion Moja na Azam abakiwe na Hela
Ndio maana nasema Simba hiyo Hela hawana labda waje na bilioni Mbili na nusu ili Yanga apewe bilioni Moja halafu Azam abakiwe na Bilion Moja na nusu sababu huwezi kuilipa Yanga Bilion Moja halafu sisi tubakiwe na Hela ndogo au tusipate Hela lazima sisi tupate Hela kubwa zaidi
Biashara ya Azam na Simba juu ya Feisal Haiwezi kufanyika yaani timu iliyonunuliwa kwa Bilion 20 unavyoona inaweza kutoa hiyo pesa?, yaani timu nzima unaipata kwa 20B, Wakati hiyo Bilion 20 hapa Azam tumenunua mabasi mawili ndio maana hizo Tetesi zipo na zitaendelea kuwepo kuwa Feisal anaenda Simba lakini Hilo haliwezi kutokea”
Mkuu WA kitengo cha habari na Mawasiliano cha Azam FC Thabiti Zakaria (Zaka Zakazi) amezungumza hayo kupitia Crown sports Asubuhi ya leo.
​Â