Kwa aina ya usajili wa Fadlu Davids namuona akifanya mabadiliko ya mfumo kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-3-3 mabadiliko yamechochewa na aina ya wachezaji ambao Simba SC wamesajili msimu huu.
Ubora wa wengi wao uko kwenye mfumo wa 4-3-3, ambao unatoa nafasi pana zaidi kwa viungo kushiriki mashambulizi na kuhimili presha ya mchezo wa kisasa.
Hata hivyo, utekelezaji wa mfumo huu mpya utategemea kama Fadlu ataona wachezaji wake wanaweza kufanya kazi hiyo vizuri, au atalazimika kurejea mfumo wake mama (wa kawaida) wa 4-2-3-1 kulingana na ufanisi wa wachezaji waliopo.
✍️Katika msimu uliopita, Fadlu alilazimika kutumia viungo wawili Ngoma na Kagoma – kwa sababu ya uhitaji wa kuimarisha safu ya ulinzi kupitia eneo la kiungo.
Ngoma alikuwa mzuri katika kutoa pasi, kusoma mchezo, na kuendesha timu, lakini hakuwa na kasi wala uwezo mkubwa wa kukaba.
Kagoma alikuwa na kasi na wepesi wa kufika kwenye maeneo ya hatari, lakini alikuwa na changamoto kwenye “game reading” na kutoa pasi sahihi za kuisogeza timu.
Hii ilisababisha Simba kuwa na uwiano wa viungo wenye ubora mahali pamoja lakini mapungufu upande mwingine.
✍️Kuingia kwa Kante: Funguo ya Mabadiliko
Usajili wa kiungo mkabaji wa kati – Kante – unampa Fadlu nafasi ya kufungua safu ya kiungo zaidi. Kante ana uwezo wa kusimama peke yake kama “single pivot” katika 4-3-3 na kulinda safu ya ulinzi bila kuhitaji msaada wa kiungo wa pili mkabaji.
Hii inampa Fadlu uhuru wa kuwaanzisha wachezaji wa ubunifu kama:
“Maema” – kucheza kama left central midfielder, akitokea upande wa kushoto na kuunganisha mashambulizi.
Ahoua – kama right central midfielder, mwenye uwezo wa kusukuma mashambulizi upande wa kulia.
Mpanzu – akicheza kama right forward katika safu ya mbele ya watu watatu, eneo ambalo ni la asili kwake.
Japo shida ni kuwa Mohamed Bajaber naye ndilo eneo lake bora nasubiri optional ya Fadlu
Tofauti na zamani ambapo Simba ililazimika kutumia mabeki wa pembeni kusukuma timu kwenda mbele, sasa Fadlu anategemea winga na viungo wa pembeni kuibeba timu kwenye mashambulizi, kwa sababu ndiko kuliko na strength