

WAKATI Yanga SC wakitajwa kukamilisha kwa asilimia 100 dili la Mohamed Hussen Zimbwe Jr aliyekuwa beki wa Simba SC na nahodha msimu wa 2024/25, Ofisa Habari wa Yanga SC, Ali Kamwe amefungukia suala la nyota huyo.
Zimbwe Jr aliwaaga mashabiki, viongozi na benchi la ufundi mara baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho hivyo ipo wazi kuwa msimu wa 2025/26 hatakuwa ndani ya Yanga SC atakuwa kwenye changamoto mpya.
Kamwe kuhusu Zimbwe Jr alisema; “Zimbwe Jr ambacho ninajua ni kwamba amewaaga mashabiki na kule alikokuwa. Kuhusu mimi kujiita jina lake ni uchaguzi tu hakuna kitu kingine,”.
Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV — usisahau ku-like, ku-comment na ku-subscribe ili uendelee kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.