MADRID: MABINGWA kihistoria wa ligi ya mabingwa Ulaya Real Madrid wametangaza kuwa mshambuliaji wao Kylian Mbappe sasa atavaa jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na ‘Legend’ wa klabu hiyo Luka Modric aliyetimkia AC Milan. Mbappe anafuata nyayo za wababe wa Real Madrid, Ferenc Puskas, Clarence Seedorf na Luis Figo ambao pia walivaa jezi namba 10.
Mbappe raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 alivalia jezi namba 9 katika msimu wake wa kwanza na Los Blancos baada ya kuwasili kutoka Paris St Germain kwa uhamisho huru.
Nshambuliaji huyo aliingia kambani mara 44 katika mashindano yote msimu wa 2024/25 licha ya kushindwa kubeba taji lolote kubwa akiwa na jezi ya Real Madrid.
Miongoni mwa wachezaji wengine mahiri waliovaa jezi namba 10 kwa Real Madrid ni Gheorghe Hagi, Michael Laudrop, Robinho na Mesut Ozil. Ikumbukwe kuwa wapinzani wao FC Barcelona walimpa winga wao Lamine Yamal jezi nambari 10 ambayo pia ina historia ya kipekee.
The post Baada ya Yamal, Mbappe nae ala 10 first appeared on SpotiLEO.