LAS VEGAS, Las Vegas jiji linalofahamika kwa sterehe na matukio makubwa ya kiburudani na michezo nchini marekani linaripotiwa kuwa mwenyeji wa droo ya Kombe la Dunia la 2026 inayotarajiwa kupangwa Desemba 5 mwaka huu.
Ripoti nyingi na tetesi juu ya hilo zilianza kuzuka mapema Jumanne katika vyombo vikubwa vya Habari kama ESPN na TUDN’Mexico vilivyosema Vegas imechaguliwa kwa droo ya kombe hili lililopanuliwa hadi timu 48 ambalo litapigwa Marekani, Canada na Mexico.
Las Vegas ndipo ilipofanyika droo ya makundi Marekani ilipokuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la 1994 huku hili la sasa likitaraji kushuhudia droo ya jumla makundi 12 yenye mataifa manne kila moja.
Ripoti ya awali ya ESPN ilisema kwamba The Sphere, ukumbi wenye viti 17,500 ambao ulifunguliwa mwaka 2023 unapewa kipaumbele kama eneo ambalo historia hiyo itaapoandikwa lakini mtandao wa The sports network uliripoti muda mchache baadae vyanzo vya Sphere vilithibitisha kwamba haitafanyika hapo.
Mwaka 1994 droo ilipangwa Las Vegas ingawa jiji hilo halikuwa mwenyeji wa mechi yoyote, hali ambayo pia imejirudia kwani hakutakuwa na mechi katika jiji hilo mwaka ujao baada ya uwanja wa Allegiant Stadium kutokidhi vigezo
The post Las Vegas kupanga makundi kombe la Dunia 2026 first appeared on SpotiLEO.