MANCHESTER: BEKI wa Manchester United Luke Shaw ameunga mkono mbinu ya adhabu inayotumiwa na meneja wa kikosi hicho Ruben Amorim kuinua morali za wachezaji katika chumba cha kubadilishia nguo akisema hali iliyokuwepo klabuni hapo wakati mwingine imekuwa mbaya sana.
Shaw ambaye amekuwepo Old Trafford tangu 2014 katika mahojiano ameiambia BBC kuwa katika muda mwingi alipokuwa klabuni hapo hali imekuwa mbaya sana kumekuwa na hali ya kukoseana hesima na hata kutomskiliza Mwalimu jambo ambalo halina afya kwa ustawi wa klabu hiyo pendwa duniani
“Hali inaweza kuwa mbaya kabisa wakati mwingine, mazingira hayana afya hata kidogo kwa maendeleo yetu tunahitaji mazingira mazuri ambayo ni chanya yenye ‘positive energy’ na furaha. Unapokuwa na vitu hivyo vyote, unajisikia huru na unajiachia zaidi”
“Ruben ameleta matakwa yake. ‘Mentality’ ni jambo kubwa sana kwenye klabu yeyote. Anazungumza mengi juu ya hili anataka tujitolee kwa 100% si vinginevyo. Ikiwa mtu anafanya 85-90%, haitoshi. Nadhani, hasa mwaka huu, ikiwa hufanyi mambo sahihi, hutacheza.” – amesema Shaw
Amorim alichukua mikoba ya kuinoa United Novemba mwaka jana na kuwataka wachezaji wa klabu hiyo kujitolea zaidi na kuona Fahari kuwa sehemu ya kikosi hicho huku akiwazuia akina Marcus Rashford na Alejandro Garnacho ambao walikuwa miongoni mwa wachezaji watano wanaotaka kuihama klabu hiyo.
Mholanzi huyo hakupepesa macho juu ya kiwango duni cha mshambuiaji wake Rashford akisema afadhali amchezeshe kocha wa makipa kuliko wachezaji wanaojitoa nusu nusu. Rashford tayari amejiunga na Barcelona kwa mkopo huku vyombo vya habari vya Uingereza vikimhusisha Garnacho kuhamia Chelsea au Aston Villa.
United, ambao walimaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita na kupoteza fainali ya Europa League dhidi ya Tottenham Hotspur, wataanza kampeni ya msimu mpya wakiwa nyumbani dhidi ya Arsenal Agosti 17.
The post Shaw : Amorim yuko sahihi first appeared on SpotiLEO.