Kamishna wa Ardhi nchini Bw. Nathaniel Nhonge (katikati), Mkurugenzi anayehisika na masuala ya Ardhi na Mipango Maalum kutoka Wizara ya Kilimo, Mazingira na Uvuvi nchini Msumbiji (MAAP) Bw. Aderito Wetela (kushoto) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prisca Lwangili wakiwa kwenye kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Ardhi na Ujumbe kutoka Msumbiji tarehe 30 Julai 2025 Jijini Dodoma.
Washiriki wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu kati ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ujumbe kutoka Msumbiji wakiwa katika kikao tarehe 30 Julai 2025 kwenye ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu kati ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ujumbe kutoka Msumbiji tarehe 30 Julai 2025 jijini Dodoma.
Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Methew Nhonge akizungumza wakati wa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu kati ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na ujumbe kutoka Msumbiji jijini Dodoma Tarehe 30 Julai 2025.
Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Ardhi na Mipango Maalum kutoka Wizara ya Kilimo, Mazingira na Uvuvi nchini Msumbiji (MAAP) Bw. Aderito Wetela akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kubadilishana uzoefu jijini Dodoma Tarehe 30 Julai 2025.
Picha ya pamoja kati ya Ujumbe kutoka Msumbiji na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati ujumbe huo wa Msumbiji ulipotembelea Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu tarehe 30 Julai 2025 jijini Dodoma. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
……………..
Na Munir Shemweta, WANMM
Ujumbe kutoka nchini Msumbiji umetembelea Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala yanaohusu sekta ya ardhi.
Ujumbe huo wa watu tisa ukiongozwa na Mkurugenzi anayehusika na masuala ya Ardhi na Mipango Maalum wa Wizara ya Kilimo, Mazingira na Uvuvi nchini Msumbiji (MAAP) Bw. Aderito Wetela umetembelea Wizara ya Ardhi tarehe 30 Julai 2025 katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Ukiwa katika ziara hiyo, ujumbe huo uliweza kubadilishana uzoefu na kupata fursa ya kupata maelezo ya namna Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inavyoendesha shughuli zake kutoka kwa Kamishna wa Ardhi Nchini Bw. Nathaniel Methew Nhonge pamoja na wakuu wa idara za wizara hiyo.
Kwa upande wake Kiongozi wa ujumbe huo Bw. Aderito Wetela alieleza namna idara inayohusika na masuala ya ardhi na mipango maalum inavyofanya kazi katika maeneo mbalimbali hususan eneo la ardhi kuanzia ngazi ya chini hadi taifa.