SUNDERLAND, Klabu ya Sunderland imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka kwa mkataba wa miaka mitatu na kurejea Premier League miaka miwili baada ya kuondoka Arsenal na kwenda Bayer Leverkusen.
Xhaka mwenye miaka 32 alikaa Arsenal kwa miaka saba kabla ya kujiunga na Leverkusen ambako alishinda Bundesliga na kufika fainali ya Europa League katika msimu wake wa kwanza. Ripoti za vyombo vya Habari nchini England zinasema Sunderland imemsajili Xhaka kwa pauni milioni 17.3.
Usajili huu wa Xaka Kwenda katika klabu hiyo mpya iliyopanda Daraja hadi EPL msimu huu unakuja wiki moja baada ya meneja wa Leverkusen Erik ten Hag kusema Xhaka alikuwa muhimu sana kwa klabu hiyo kumwachilia.
“Ninajivunia kuwa hapa. Nilipozungumza na Klabu, nilifurahi na nilihisi nguvu, na mawazo ambayo watu wote na wachezaji wanayo,” Xhaka alisema katika taarifa ya klabu.
Xhaka ambaye amecheza mechi 225 za Premier League akiwa na Arsenal, alishinda Kombe la FA mara mbili akiwa na timu hiyo ya Kaskazini mwa London.
Sunderland wanaanza kampeni yao za ligi kuu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya West Ham United mnamo Agosti 16
The post Xaka atua Sunderland first appeared on SpotiLEO.