Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Queens, Precious Christopher amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Yanga Princess wenye kipengele cha kuongeza kama atafanya vizuri.
Msimu uliopita Precious aliichezea Simba Queens akifunga mabao mawili na asisti tatu kwenye mechi 18 za Ligi Kuu alizocheza.
Kwa mara ya kwanza Precious alitambulishwa Yanga msimu wa 2021 akitokea kwao Nigeria na akaicheza kwa misimu miwili na uliopita akaenda kwa wapinzani wao Simba.