LONDON: MAHAKAMA ya usuluhishi wa michezo (CAS) imesema itaanza mchakato wa ndani wa kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Crystal Palace dhidi ya shirikisho la soka barani ulaya (UEFA), klabu ya Nottingham Forest na Olympique Lyon mnamo Agosti 8 mwaka huu.
Crystal Palace ilishushwa hadi Conference league na Bodi ya Udhibiti wa Fedha ya Klabu ya UEFA katika kesi ya umiliki pacha wa klabu huku hiyo na Olympique Lyon ya Ligue 1 huku wenzao hao wakiruhusiwa Europa League
Klabu hiyo ya London ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo huku CAS sasa ikithibitisha kuwa itasikiliza kesi hiyo mwezi ujao. Nottingham Forest, ambao walimaliza katika nafasi ya saba kwenye Premier League watachukua nafasi ya Palace kwenye Europa ikiwa rufaa yao itashindwa.
Palace walikuwa wamefuzu kwa Europa league baada kushinda Kombe la FA msimu uliopita, huku Lyon wakifika kinyang’anyiro hicho kwa kumaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligue 1. Hata hivyo, klabu hiyo ya Ufaransa iliruhusiwa kutokana na kumaliza nafasi ya juu kwenye ligi. CAS inatarajia kutoa uamuzi tarehe 11 Agosti.
The post CAS kufungua ‘faili’ la Palace mwezi ujao first appeared on SpotiLEO.