DICKSON JOB NICKSON , One of the best Defender! Kutoka Morogoro akiwa ndani ya jezi ya Mtibwa Sugar hadi Kariakoo Jijini Dar es Salaam akiwa kwenye uzi wa Young Africans mpaka hivi sasa, ni wakati ule ambao watu wengi hawakuamini kama anapenya kikosi cha kwanza lakini alifika na kufanya hivyo
Ni wakati ule ambao Kelvin Yondan ameondoka Jangwani na jezi Namba Tano inasubiri mtu lakini Job alivaa, watu wakaamini ubongo na miguu yake hadi leo yupo katika ubora wake, ni wakati ule yupo kwenye timu inayoishi kwa presha hasa kushinda mashindano ya ndani na kwenda kufanya vizuri michuano ya CAF
Jangwani walimpa nafasi tu na kilichofuata ni historia, ukuta ule ambao Bakari Nondo na Dickson Job kama wachezaji wazawa walisimama vizuri, wakati ule maswali yalikuwa mengi sana namna gani wanaenda kulinda mstari wa ulinzi lakini walivuka vizuri hadi leo Dickson Job anapata nafasi kubwa uwanjani
Simply, klabuni anavaa kitambaa cha unahodha kama Mwamnyeto hayupo uwanjani, huyu ni mchezaji mzawa mwenye muendelezo mzuri kwa sasa uwanjani na sifa ya kuwa kiongozi kwake ipo juu, ni nzuri sana kubaki na quality ya aina hii kikosini kama unataka kushindana! Top player for Young Africans 🫡
Mwandishi @officialevodiusoscar_
​Â