HONGKONG: KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta amesema mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Viktor Gyokeres anaweza kuichezea Arsenal kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa dabi ya London kaskazini itakayopigwa mbele ya mashabiki 50 000 wa jiji la Hong Kong saa 8 mchana wa leo.
Mshambuliaji huyo raia wa Sweeden aliyeigharimu Arsenal ya dola milioni 67 alihudhuria mazoezi ya wazi ya Arsenal katika uwanja wa Kai Tak ambapo Arsenal itamenyana na Tottenham katika pambano la kwanza la mahasimu hao nje ya nchi yao England.
Gyokeres alijiunga na Arsenal katika ziara yao ya Asia siku tatu zilizopita baada ya kusajiliwa kutoka Sporting Lisbon lakini kocha Arteta anasema atapata muda uwanjani ikiwa timu ya madaktari aa klabu itathibitisha kuwa yuko tayari.
“Naelewa ameanza mazoezi jana na juzi tena kidogo. Tutamtazama usiku wa leo ikiwa timu ya matabibu watafurahishwa na hali yake basi atacheza, kuna uwezekano.” – Arteta aliwaambia waandishi wa habari.
Gyokeres mwenye umri wa miaka 27 aliisaidia Sporting kutwaa ubingwa wa Ureno msimu uliopita akiwa na mabao 39 na kugonga vichwa vya habari duniani alipofunga hat-trick ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City.
The post Gyokeres kuanza na Dabi ya London first appeared on SpotiLEO.