Unaweza kuliita pigo kuu kwa timu ya taifa ya Kenya, maarufu kama ‘Harambee Stars’ inayoshiriki michuano ya CHAN 2024, baada ya kiungo wao fundi Mohammed Bajaber kujiunga na Simba Sports Club ya Tanzania kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano mingine ya kimataifa.
Bajaber anadaiwa kujiunga na klabu ya Simba ambayo iko kambini nchini Misri, kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Hii inamaanisha kuwa, Bajaber atakosa michuano ya CHAN 2024, ambayo ni maalumu kwa wachezaji wanaoshiriki ligi za ndani.