

Mashabiki wa mitandao ya kijamii wameachwa midomo wazi baada ya mrembo Lovless Tarimo, mwanamke mashuhuri kwa mwili wake wa misuli na mazoezi makali ya kubeba vyuma, kutangaza kuwa ni mjamzito. Lovless, ambaye amekuwa kivutio cha wengi kutokana na ujasiri wake kuvunja mitazamo ya kijinsia kwenye ujenzi wa misuli, alichapisha picha zake pamoja na ujumbe wakua ni mjamzito huku akionekana mwenye furaha na utulivu.
Wengi walieleza mshangao wao, wakisema hawakutegemea kama anaweza kubeba mimba kutokana na mwonekano wake wa kimchezo. Hata hivyo, Lovless ameendelea kupokea pongezi na kutajwa kama mfano bora wa nguvu ya mwanamke wa Kiafrika anayeweza kuwa chochote — mwenye misuli na uzazi pia.