Klabu ya Simba SC imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji kutoka Senegal, Alassane Kanté, usiku wa Julai 30, 2025.
Kanté, mwenye umri wa miaka 24, ni mchezaji wa nafasi ya kiungo wa kati (central midfield) mwenye urefu wa mita 1.85. Anajiunga na Simba akitokea CA Bizertin ya Tunisia ambako aliwika kwa uwezo wake wa kutawala eneo la kati.
Usajili wake ni ishara ya dhamira ya Simba SC kuimarisha safu ya kiungo kuelekea msimu mpya. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu kumuona Kanté akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na jezi nyekundu ya Simba.