THESSALONIKI: WINGA wa zamani wa mabingwa wa Laliga FC Barcelona Carles Perez ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Aris Thessaloniki ya Ugiriki amekosekana katika mchezo muhimu wa kufuzu kwa Conference league baada ya kushambuliwa na mbwa katika sehemu zake za siri kama vinavyoripoti vyombo vya habari vya vya Hispania.
Imeripotiwa kuwa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akitembea na mbwa wake alipong’atwa sehemu za siri na mbwa mwingine wakati wa jaribio la kuwatenganisha wanyama hao waliokuwa wakipigana. Tukio hilo lilimfanya apate jeraha kubwa akihitaji matibabu zaidi hospitalini.
Perez alikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza dhidi ya timu ya nyingine ya Ugiriki Araz-Nakhchivan katika mkondo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu kwa Conference League na kupokea kichapo cha mabao 2-1 hata hivyo ripoti zinasema hatakuwa ‘fiti’ kwa mechi ijayo.
Perez ni zao la akademi ya Barcelona La Masia na alicheza katika timu ya wakubwa ya Barcelona kwa mara ya kwanza mwaka 2019 akifunga bao katika mchezo wake wa kwanza wa La Liga kisha kupelekwa kwa mkopo AS Roma iliyomununua na kumtoa kwa mkopo Celta Vigo kabla ya klabu hiyo nayo kumpeleka kwa mkopo Aris aliko hadi mkasa huu ulipomkuta.
The post Winga ang’atwa na mbwa sehemu za siri first appeared on SpotiLEO.