Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Watanzania, kujitokeza kwa wingi kwenye mechi ya ufunguzi ya michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN2024 ambapo Tanzania itacheza dhidi ya Burkina Faso.
Rais Samia amesema hayo leo kwenye ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC) Ubungo, Dar es Salaam na kubainisha kwamba Watanzania wana imani kubwa na wachezaji wanaounda kikosi cha Taifa Stars na kwamba kombe likibaki Tanzania wajue wana tuzo yao kutoka kwake.
Aidha Mkuu huyo wa Nchi amewataka Watanzania kuwakaribisha Wageni wanaokuja kushiriki katika mashindano hayo yatakayofunguliwa kesho Agosti 02, 2025 kwa kuhimiza Utulivu, Heshima, Ukarimu na kwa Amani.