Taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limetangaza rasmi kuingia makubaliano ya udhamini wa miaka minne na mabingwa wa Hispania FC Barcelona wenye thamani ya Bilioni 134 kwa ajili ya kuvutia utalii na kuhamasisha uwekezaji kutoka nje ya Taifa lao.
Kutokana na mkataba huo wachezaji wa Barcelona wataanza kuvaa jezi za mazoezi zenye maandishi “DR Congo “Moyo wa Afrika” kuanzia msimu ujaohuku pia ikihusisha kambi za mafunzo kwa vijana, maonyesho ya utamaduni wa Kongo kwenye uwanja wa Camp Nou, pamoja na programu mbalimbali za michezo.