RASMI Simba SC imemalizana na mshambuliaji wa mabao Jonathan Sowah ambaye alikuwa mali ya Singida Black Stars na sasa atakuwa mali yao.
Ikumbuwe kwamba Julai 31 2025 Simba SC ilitambulisha wachezaji wawili wapya ambao ni Morice Abraham alitambulishwa ndani ya Simba SC Julai 31 2025 na Hussein Daudi Semfuko alitambulishwa Simba SC, Julai 31 2025 kuwa ni mali ya Simba SC. 2024/25 alikuwa akicheza Coastal Union ya Tanga.
Jonathan Sowah alikuwa ndani ya Singida Black Stars ni raia wa Ghana ambaye msimu wa 2024/25 akiwa na Singida Black Stars alifunga jumla ya mabao 13 kwenye ligi akiwa ni ingizo jipya dirisha dogo.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC aliweka wazi kuwa Sowah ni mshambuliaji mzuri na ana kazi kubwa uwanjani hivyo kumpata ni faida.