šNIRC:Dodoma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kasim Majaliwa, amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt.Gerald Mweli kuhakikisha kuwa Wizara hiyo, kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, inashirikiana na sekta nyingine za umma ili kuhimiza matumizi ya teknojia za kisasa za Umwagiliaji, ikiwa ni pamoja kuhamasisha uwekezaji kutoka kwa wadau wa sekta binafsi wenye uwezo wa kuleta teknojia hizo nchini.
Pia Majaliwa amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa kwa kuhakikisha kunakuwapo mitambo na teknolojia za kisasa za Umwagiliaji katika maonesho hayo, ambazo zitatumika katika kaboresha sekta ya kilimo nchini na matumizi mengine ikiwemo viwanja vya michezo.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo katika maonesho ya nanenane 2025, alipotembelea eneo la Umwagiliaji ikiwemo kijiji cha mitambo ya Umwagiliaji, lengo likiwa ni kukagua mitambo mbalimbali na uwekezaji wa serikali uliofanywa katika sekta hiyo.
Majaliwa amesema, kazi kubwa imefanyika katika Umwagiliaji hivyo ni muhimu Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha wanashirikisha sekta nyingine kupanua wigo wa huduma za umwagiliaji nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa.
ā Umwagiliji huu mdogo mdogo unahitajika hata na Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo lengo ni kuhamasisha ujenzi wa viwanja nchi nzima kwa kuotesha majani halisi badala ya āartificialā uwanja kama wa kwetu wa Dodoma Mkuu wa mkoa una ukame sana tukipata mitambo hii ya umwagiliaji itafungua milango,āamesema.
Amesema ili kupata mafanikio ni lazima kuwa na msukumo wa pamoja kwa Makatibu wakuu na taasisi nyingine ikiwemo Magereza, Jeshi la Kujenga Taifa na taasisi binafsi zinazojihusisha na kilimo kuwezeshwa kuwa na mitambo ya kilimo cha Umwagiliaji lengo likiwa ni kuwa na uhakika wa chakula.
āPia wakulima binafsi wenye mashamba makubwa akiwemo yule wa Iringa tuone namna ya kuwawezesha,āamesema.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Gerald Mweli, amesema Wizara inashirikiana na uongozi Mkoa wa Dodoma kupanga vijana ili waweze kuendelea na uzalishaji katika maeneo ya kilimo mkoani humo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa amesema Tume imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, hususani ya matumizi ya teknolojia za kisasa za Umwagiliaji kupitia viwanja hivyo hata baada ya maonesho.
āKijiji hichi cha mitambo na teknolojia nyingine za Umwagiliaji zitaendelea kuwepo katika viwanja hivi vya nane nane, Nzuguni Mkoani Dodoma na Tume imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wakulima ili wajue huduma na uwekezaji unaofanywa na Serikali katika Umwagiliji,āamesema.
Akitoa maelezo ya kitaalamu Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Dodoma, Oswald Urasa amemweleza Waziri Mkuu kuwa mitambo hiyo ya Umwagiliaji ikiwemo wa
(CENTER PIVOT), ambao unauwezo wa kumwagilia hekta tano, sawa na ekari 12.5 ndani ya saa 24 na ambapo mtambo huo umeunganishwa na mifumo ya kutambua kiwango cha unyevu kwenye ardhi, mfumo wa kuweka mbolea na mfumo wa kutabiri hali ya hewa.
Ā