
Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Makete, Festo Richard Sanga, ameongoza katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwania tena nafasi ya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Katika matokeo yaliyotangazwa rasmi, Sanga alipata kura 4,104, akimshinda kwa tofauti kubwa Dr. Toba Nguvila aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 2,359. Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mfanyabiashara Award Mpandilla aliyepata kura 946.
Wagombea wengine waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni:
Prof. Norman Sigalla, aliyepata kura 103
Selina Msigwa, aliyepata kura 21
Kwa ushindi huo, Festo Sanga ameonesha kuwa bado ana uungwaji mkono mkubwa ndani ya chama katika jimbo hilo, na sasa anasubiri uteuzi wa mwisho kutoka kwa mamlaka za juu za CCM ili kujua hatma yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.