BANK of Africa Tanzania yashiriki katika maadhimisho ya miaka 26 ya Mfalme Mohammed VI wa Ufalme wa Morocco. Tukio hilo la lilifanyika jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha viongozi wa kidiplomasia, mabalozi kutoka nchini mbalimbali wanaowakilisha nchini zao hapa Tanzania, wafanyabiashara, na wawakilishi mbalimbali katika kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Bank of Africa Tanzania ni kampuni tanzu ya BANK OF AFRICA Group, mtandao wa kifedha wa Kiafrika wenye makao yake makuu nchini Morocco, ukiwa na mtandao katika nchi 17 za Afrika pamoja na pia nchini Ufaransa. BANK OF AFRICA – BMCE, benki ya pili kwa ukubwa miongoni mwa benki binafsi nchini Morocco.
Katika tukio hili, benki ilisisitiza tena dhamira yake ya kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Morocco kupitia ushirikiano wa kifedha na kitamaduni.
Maadhimisho haya yalidhihirisha uhusiano unaokua kwa kasi kati ya mataifa haya mawili, ambapo Bank of Africa Tanzania inachukua nafasi ya kiunganishi kati ya Afrika Mashariki na Afrika Kaskazini, kwa lengo la kuchochea ushirikiano wa kiuchumi na ustawi wa pamoja.
Bank of Africa Tanzania itaendelea kushiriki katika kuendeleza maendeleo ya kikanda kupitia ushirikiano wa kimkakati barani Afrika na kwingineko.
Mgeni rasmi alikuwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MP), Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki
