Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Janeth Mayanja akipata ufafanuzi kuhusu majukumu yanayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka kwa Mkuu wa,Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi hiyo, Bi. Sarah Kibonde wakati alipotembelea Banda la Ofisi hiyo katika maonesho ya 32 ya kitaifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Jumatatu Agosti 4, 2025 viwanja vya Nanenane Nzuguni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Bw. Mnyikah Hassan akieleza jambo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sarah Kibonde wakati alipotembelea Banda la Ofisi katika maonesho ya 32 ya kitaifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Agosti 4, 2025 viwanja vya Nanenane Nzuguni. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Janeth Mayanja.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Mhe. Janeth Mayanja akionesha baadhi ya nakala ya kitabu cha miaka 60 ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Sarah Kibonde wakati alipotmbelea banda la ofisi hiyo katika maonesho ya 32 ya kitaifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo Agosti 4, 2025 viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, Bw. Mnyikah Hassan akipokea nakala ya nyaraka mbalimbali kutoka kwa Mkuu wa Kitengo Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sarah Kibonde muda mfupi baada ya ,kutembelea banda la ofisi hiyo leo Agosti 4, 2025 wakati wa maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Mhe. Janeth Mayanja (katikat), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma Bw. Mnyikah Hassan wakiwa picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Selikalini Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sarah Kibonde muda mfupi baada ya kutembelea banda la Ofisi hiyo leo Agosti 4, 2025 katika maonesho ya 32 ya kitaifa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni.
Mkuu wa Kitengo Serikalini Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Sarah Kibonde akimkabidhi Afisa Habari wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania, Bw. Boaz Mazigo nyaraka za machapisho mbalimbali yanayozalishwa na Ofisi hiyo wakati alipotembelea banda la ofisi hiyo leo Agosti, 2025 katika maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni.
Mkurugenzi wa kitengo cha manunuzi na Ugavi Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Juliana Mkalimoto (wa tatu kulia mwenye miwani) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Sarah Kibonde wakati alipotembelea banda la Ofisi hiyo leo Agosti 4, 2025 katika maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.
….
Ofisi ya Makamu wa Rais imeombwa kutafuta makampuni makubwa duniani kuja nchini ili kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuibua fursa za uwekezaji zilizopo katika malighafi za taka.
Rai hiyo imetolewa leo Jumatatu (Agosti 4, 2025) jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Janeth Mayanja wakati alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maonesho ya 32 ya Kitaifa ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane Nzuguni.
Mhe. Mayanja ameeleza kuwa mataifa yaliyoendelea yamepiga hatua kubwa katika usimamizi wa biashara ya taka na hivyo kushauri Ofisi ya Makamu wa Rais kuangalia utaratibu wa kuwashirikisha wadau wengi zaidi ikiwemo makampuni makubwa ya taka kuja nchini na kuwekeza katika miradi hiyo ili kuibua fursa kwa wananchi.
“Ushiriki wa wadau ikiwemo makampuni makubwa ya biashara ya taka ni muhimu sana kwa wakati huu kuja nchini na kuona uwezekano wa kushirikiana na Serikali za mitaa katika kubadilisha malighafi za taka kuwa fursa za ajira na kiuchumi kwa wananchi wetu”
Aidha amepongeza jitihada zilizofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuandaa na kuzindua Mkakati wa Usimamizi wa Taka wa mwaka 2025 kwani hatua ni muhimu katika kuhakikisha malighafi taka zinaibua fursa za kiuchumi sambamba na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Mhe. Mayanja ameongeza kuwa Mkakati huo umekuja katika wakati mwafaka hususani katika kipindi hiki ambacho serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha ujasiramali wa mazingira kupitia biashara ya kaboni na malighafi taka.
Kuhusu muungano, Mhe. Mayanja amehimiza Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea kutoa elimu hiyo kwa makundi mbalimbali ya kijamii hususani vijana ambao wamekuwa mstari wa mbele kujifunza masuala mbalimbali kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.
“Elimu kuhusu mambo 22 ya Muungano ni hatua moja muhimu ya kuwaeleza wananchi kuhusu chimbuko na misingi ya Muungano wetu, nawasihi tuendelee kuwaelimisha vijana na watoto masuala ya Muungano kupitia majukwaaa ya mitandao ya kijamii” amesema Mhe. Mayanja.
Aidha amesema kuwa juhudi kubwa zimeendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha Muungano na usimamizi endelevu wa hifadhi ya mazingira nchini na hivyo upo umuhimu= wa mafanikio hayo kutangazwa kwa umma na jamii kwa ujumla.
Maonesho ya kilimo, wafugaji na wavuvi mwaka 2025 yamebeba kauli mbiu isemayo “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”