NIGERIA: GAVANA wa Jimbo la Ondo Lucky amemzawadia beki wa Super Falcons, Oluwatosin Demehin zawadi ya Naila milioni 30 na nyumba yenye samani zote za ndani iliyopo katika eneo la Akure nchini Nigeria.
Haya yanajiri kufuatia uchezaji bora katika Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) 2024 nchini Morocco, ambapo Nigeria ilinyakua taji hilo kwa ushinid wa bao 3-2.
Gavana huyo alimpokea Demehin katika Ikulu ya Serikali ya Jimbo la Ondo jana, akimmwagia sifa nyota huyo mzaliwa wa Akure ambaye alicheza kila dakika ya mechi sita za Nigeria katika mashindano hayo.
Demehin, ambaye anacheza Fenerbahçe ya Uturuki, aligonga vichwa vya habari alipofunga bao lake la kwanza la kimataifa wakati Nigeria ilipoiangamiza 5-0 Copper Queens ya Zambia katika mchezo wa robo fainali.
Bao hilo liliweka alama maalum kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, ambaye alipanda daraja kutoka Falconets na kuwa tegemeo katika timu ya taifa ya wakubwa.
Wazawa wengine wawili ambao walikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda WAFCON cha Nigeria, afisa wa habari wa timu Mary Akinsola na katibu wa timu Mary Oduboku, pia walitunukiwa pesa taslimu Naila milioni 15 kwa kutambua michango yao katika kukuza soko la Nigeria.
The post Gavana Super Falcons atoa milioni 30 first appeared on SpotiLEO.