Kiungo mshambuliaji kutoka DR Congo Elie Mpanzu amemaliza utata uliokua unawasumbua mashabiki na wanachama wa Simba, kuhusu hatma yake klabuni hapo kwa kutonga kambini Ismaili, Misri mapema leo Jumanne.
Kabla ya kutua kambini hapo taarifa za utata zilidai huenda Mpanzu asingerejea klabuni hapo kufuatia sintofahamu iliyouhususha uongozi wake na ule wa Simba.