DAR ES SALAAM: Baada ya kuwa pamoja kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, sasa msanii Marioo na mpenzi wake Paula wapo mbioni kuchukua hatua kubwa zaidi ya maisha yao ya mahusiano hadi ndoa.
Katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya ‘Girlfriend’, Paula alitumia ukurasa wake wa Instagram kushiriki ujumbe uliogusa mioyo ya wengi.
Akiandika:”Apparently, this was my last girlfriend’s day… Babe said next year I’ll be celebrating as a wife.”
Kauli hiyo imeibua hisia kali miongoni mwa mashabiki, wengi wakichukulia kama tangazo rasmi kuwa Marioo amemvisha Paula pete ya uchumba au angalau kumpa ahadi ya ndoa.
Wawili hao wameendelea kudhihirisha kuwa penzi lao linazidi kuimarika kila uchao, na sasa mashabiki wanasubiri kwa shauku kubwa kuona sherehe ya harusi inayotarajiwa kufanyika mwakani.
Pongezi na salamu za heri zimeendelea kumiminika kwa wapenzi hao kupitia mitandao ya kijamii, huku wengi wakitafsiri ujumbe huo kama ishara ya mwanzo mpya katika maisha yao ya kimapenzi.
The post Marioo kumuoa Paula? ujumbe huo wazua gumzo first appeared on SpotiLEO.