MSANII kutoka nchini Nigeria Rudeboy (King Rudy ), ametuma ujumbe mzito kupitia Instagram Story yake kwa wasanii wapya kwenye tasnia ya muziki.
Ameeleza wasiwasi wake juu ya tabia ya baadhi ya vijana kurekodi video huku wakivuta bangi, bila kujali afya zao.
“Wimbo hata haujaanza sekunde 20, tayari mnaanza kuvuta bangi kwa ajili ya kamera? Mnaonekana wagonjwa!” ameandika Rudeboy.
Amesema kuwa baadhi yao wanatumia fedha nyingi kwa bangi lakini wameshindwa kujijali kwa kula vizuri au hata kula kabisa.
Kwa Rudeboy, sigara au bangi siyo “swag”, bali ni ishara ya presha ya kutaka kuonekana maarufu kwa nguvu. Ametoa wito kwa wasanii wachanga kuweka afya na akili mbele ya kila kitu, ili safari yao ya muziki iwe ya muda mrefu na yenye tija.
The post Rudeboy: Wasanii acheni bangi first appeared on SpotiLEO.