Klabu ya Dodoma Jiji imemsajili kiungo wa Tabora United Mkongomani Nelson Munganga.
Munganga amejiunga na kikosi hicho kwa miaka miwili na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa kikosi hicho Moses Mpunga amethibitisha.
Munganga ni mchezaji mwingine aliyesajiliwa na kikosi hicho baada ya jana mchana Dodoma Jiji kutangaza kumsajili mlinzi wa kushoto Miraji Abdallah.