ELLIE Mpanzu, winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids amewasili kambini rasmi Agosti 5 2025 kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za watani wa jadi wa Simba SC ambao ni Yanga SC kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
Inaelezwa kuwa alichelewa kambini kutokana na matatizo ya kifamilia jambo ambalo lilimfanya akachelewa kujiunga na Simba SC kambini nchini Misri.
Tayari kikosi cha Simba SC kimeanza maandalizi mapema kabla ya ligi kuanza. Ligi inatarajiwa kuanza kushika kasi Septemba 16 2025 ikiwa ni mwanzo wa msimu mpya.
Baada ya kuripoti kambini, Mpanzu amekabidhiwa vifaa vya kazi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na alipata muda kuwasilimia wachezaji wa timu hiyo.