Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Taasisi za umma na binafsi waadhimisha siku ya mikoko duniani kwa kupanda miche takribani 1,000 ya miti ya Mikoko eneo la Kilongawima lililopo pembezoni mwa fukwe ya ‘Mbezi beach’ Halmashauri ya Kinondoni Manispaa ya Jijini Dar es.
Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji wa miche hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amewataka wananchi kulinda na kithamini mikoko kwani Inamanufaa mkubwa katika kulinda ikolojoa ya bahari na viumbe hai waishio majini.
Naye Dkt.Rose Sallema, Meneja wa Tafiti za Mazingira (NEMC) alipozungumza alisema mikoko ni rasilimali ya bahari inayotakiwa kutunzwa kwani inafaida kiuchumi,kijamii na kimazingira.
Naye Mkurugenzi Msaidizi, Maendeleo ya Misitu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ndugu. Seleboni Mushi alipozungumza aliitaka jamii kuzingatia Uhifadhi wa misitu ya Mikoko kwani husaidia kuhifadhi fukwe na hewa ukaa hivyo kusaidia kuhimili mabadiliko ya tabianchi.
Ameongeza kuwa ni Hifadhi ya viumbe hai na husaidia jamii hasa za Pwani katika kujipatia kipato.
Taasisi zilizoshiriki Maadhimisho hayo ni pamoja na TFS, WWF, IUCN, Wetland, Mwambao International Wawakilishi kutoka maeneo ya Pwani ya Kibiti, Kilwa na Mafia.