Mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amesisitiza kwamba ana njaa ya kupata mafanikio makubwa msimu huu.
Mbappe ameyasema hayo kupitia chapisho lake kwenye mtandao wake wa Instagram.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alisema:
“Msimu mpya. Nina njaa ya kufanya jambo kubwa, Twende sote pamoja, Madridistas. HALA MADRID.”
Nahodha huyo wa Ufaransa alijiunga na Real Madrid kutoka Paris Saint-Germain mwaka jana.