Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kigoma Malima (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere Mkoani Morogoro, tarehe 04 Agosti 2025
…………
Na. Mwandishi Wetu Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kigoma Malima ametembelea banda la Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika maonesho ya Nane Nane yanayofanyika katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere Mkoani Morogoro kwa Kanda ya Mashariki inayojumlisha Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga na Morogoro. Katika banda hilo,
Mhe. Malima ameishukuru TMDA kwa huduma inayotoa kwa wananchi na hivyo ameitaka kuendelea kuimarisha mifumo ya udhibiti bila kuchoka.
Na kuongeza kuwa, TMDA inafanya kazi kubwa sana katika kulinda afya ya jamii kwa kutumia mifumo yake thabiti iliyowekwa huku akiitaka kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya dawa kwa kipindi chote cha maonesho hayo ya Nane Nane sambamba na kuangazia matumizi holela ya dawa.
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa TMDA, Bi. Gaudensia Simwanza amesema TMDA inashiriki katika maonesho hayo Nane Nane katika Kanda zote nchini.
“Tupo katika maonesho ya Nane Nane 2025 katika Kanda zote ikiwemo viwanja vya Nzuguni Dodoma Kanda ya Kati, Viwanja vya Mwakangale Mbeya Nyanda za juu, Viwanja vya Nyakabindi Mkoa wa Simiyu, viwanja vya Themi Mkoa wa Arusha
Pia viwanja vya Ngongo Mkoa wa Lindi, Viwanja vya Fatma Mwasa mkoa wa Tabora na viwanja vya Nyamhongolo Mkoa wa Mwanza kwa Kanda ya Ziwa.