Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa klabu ya Le Havre inayoshiriki Ligi kuu nchini Ufaransa.
Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza kwenye mataifa manne 5 Barani Ulaya akianzia Ubeljiji,Uingereza,Uturuki,Ugiriki na Ufaransa.