ROME: Waamuzi wa Serie A wataanza kutangaza maamuzi ya VAR moja kwa moja viwanjani na kwenye televisheni kuanzia msimu ujao baada ya bodi ya waamuzi wa ligi hiyo kufanya uamuzi huo muhimu kwa mustakabali wa mashabiki wa uwanjani
Akizungumza na vyombo vya Habari jijini Roma Gianluca Rocchi, mkuu wa waamuzi wa Serie A aliitaja hatua hiyo kama ni hatua kubwa katika mawasiliano kati ya waamuzi na mashabiki akisema lengo ni kufanya maamuzi ya waamuzi kwa haraka na kwa uwazi zaidi.
“Tulifanya kosa msimu uliopita kwa kupunguza mbinu zetu za mawasiliano. Wakati mwingine tulijaribu kulilinda Kundi hili (waamuzi) badala ya kueleza uhalisia. Tayari tuna kundi teule la waamuzi na tunataka kuhakikisha kuna lugha inafanana iwezekanavyo ili maamuzi yawe wazi kwa umma” – Rocchi alisema.
Huu unakuwa muendelezo wa ligi mbalimbali barani Ulaya kuchukua hatua ya waamuzi kueleza maamuzi kwa umati ulio uwanjani kama ambavyo watazamaji wa televisheni walivyokuwa wakipata fursa hiyo. Uamuzi kama huo umetajwa pia England na Ujerumani
Ikumbukwe katka Kombe la Dunia la Klabu lililomalizika hivi majuzi waamuzi walikuwa wakitangaza uwanjani maamuzi ya VAR. Msimu mpya wa soka la Ulaya unaanza rasmi Agosti 13 huku ligi ya Serie A ikianza cheche zake Agosti 23
The post Serie A kutangaza maamuzi ya VAR uwanjani msimu ujao first appeared on SpotiLEO.