MRITHI wa kitambaa cha unadhoa ndani ya kikosi cha Simba SC kwa sasa anatafutwa mara baada ya beki huyo wa kushoto kutambulishwa Jangwani.
Zimbwe Jr alikuwa nahodha wa Simba SC msimu wa 2024/25 mkataba wake ulipogota mwisho hakuongeza kandarasi nyingine hivyo katambulishwa Jangwani akiwa mchezaji huru.
Inatajwa kuwa mabosi wa Simba SC na benchi la ufundi linafanyia kazi orodha ya wachezaji waliopo ndani ya Simba SC huku jina la Shomari Kapombe likitajwa kuwa miongoni mwa majina yanayopewa kipaumbele.
Mbali na Kapombe, Mzamiru Yassin na Ellie Mpanzu ni miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kuwa kwenye hesabu za mastaa hao kupewa hadhi ya kuvaa kitambaa cha unahodha.