Kampuni ya GSM Group kupitia kwa mshirika wake Kampuni ya Vifaa vya Umeme vya Haier leo wameingia Mkataba wa udhamini na Yanga SC kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mkataba huo wa miaka mitatu wa Yanga na Haier una thamani ya Tsh Bilioni 3.3 hivyo kwa sasa Haier logo yake itaonekana katika begi la jezi za Yanga katika michuano ya ndani.