NEW YORK: Mwana wa mwimbaji maarufu wa muziki wa pop kutoka Canada Justin Bieber, Jack Blues ameanza kuonekana rasmi kwenye video ya muziki wake.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alitoa picha za rangi nyeusi na nyeupe za wimbo wa ‘Yukon’, wimbo wa pili kutoka katika albamu yake iliyotolewa hivi karibuni aliyoiita ‘Swag’.
Picha hiyo pia inamuonesha mke wa Bieber, Hailey Bieber na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miezi 11 wakiwa pamoja naye.
Video ya wimbop huo iliyoongozwa na Cole Bennett-ambaye anachumbiana na rafiki wa karibu wa Hailey Camila Morrone inaanza kwa kumuonesha Justin akiwa amemshika Jack kwenye mapaja yake wakiwa katika safari ya boti, huku miguu ya motto huyo ikicheza kwenye maji.
Video hiyo pia inamuoesha Justin akibusu vidole vya miguu vya Jack huku mama yeka Hailey akimpapasa mwana wao huyo baharini.
Video hiyo inaongeza mkusanyiko unaokua wa matukio ambayo Bieber ameshiriki akimshirikisha mwanawe.
Mwezi uliopita, mwimbaji Baby alichapisha picha za nyuma ya pazia kutoka kwa kipindi cha kurekodi ambapo Jack alionekana amesimama karibu na meza ya kahawa huku wanamuziki wakipiga gitaa karibu naye.
Video ya ‘Yukon’ inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya wanandoa hao kumkaribisha mtoto wao wa kwanza. Justin na Hailey walifunga ndoa mwaka wa 2018 na kuweka upya viapo vyao Mei 2024 wakiwa likizoni Hawaii. Mwezi huo huo, walitangaza ujauzito wa Hailey, na Jack aliyezaliwa Agosti, mwaka jana.
“Kuwa baada ya kuzaa ndio wakati nyeti zaidi ambao nimewahi kupitia maishani mwangu, na kujifunza toleo jipya la mimi mwenyewe ni ngumu sana,” amesema.
“Na hilo ndilo jambo: Nina maisha halisi. Maisha yangu halisi ni kwamba ninaamka na familia yangu nzuri na mwanangu na marafiki zangu na nina watu wanaonijua na kunipenda na ninawapenda,” ameongeza.
The post Justin Bieber aanza na mtoto wake kwenye video first appeared on SpotiLEO.